15/10/2026
Leo, tarehe 15 Oktoba 2026, Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku ya Kunawa Mikono Duniani, siku maalum inayolenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kunawa mikono kwa usahihi kwa kutumia maji tiririka na sabuni.
Kunawa mikono ni moja ya njia rahisi, salama na yenye gharama nafuu ya kujikinga na maambukizi ya magonjwa mbalimbali. Mikono inaweza kuwa chanzo cha kusambaza vijidudu kutoka sehemu moja kwenda nyingine, hasa tunapogusa uso, chakula au vitu vinavyotumiwa na watu wengi.
Kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni husaidia kuondoa vijidudu vinavyoweza kusababisha magonjwa k**a kuhara, kipindupindu, maambukizi ya njia ya hewa na magonjwa mengine ya kuambukiza. Hivyo, kunawa mikono ni sehemu muhimu ya usafi binafsi na kinga ya afya ya familia na jamii.
Ni muhimu kunawa mikono kabla ya kuandaa au kula chakula, baada ya kutumia choo, baada ya kumhudumia mtoto, baada ya kukohoa au kupiga chafya, baada ya kushika taka, na wakati wowote mikono inapokuwa michafu.
Wazazi, walezi, walimu na viongozi wa jamii wanahimizwa kuwa mfano kwa watoto na jamii kwa kuhakikisha kunawa mikono kunakuwa sehemu ya utamaduni wa kila siku. Pia, ni muhimu kuweka vituo vya kunawia mikono vyenye maji tiririka na sabuni katika maeneo ya nyumbani, shule, vituo vya afya, masoko na maeneo mengine ya umma.
Kumbuka: Mikono safi ni kinga dhidi ya magonjwa. Nawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, linda afya yako na afya ya jamii.