Health_farm_tz

Directions Website Contact the business

Health_farm_tz Elimika, Hamasika, Chukua Hatua Kabla Mwili Haujachoka! Work with us 👇🏽
📩[email protected]
(1)

Health_farm_tz inapatikana kwenye Instagram, WhatsApp na Facebook kwa jina Hilo hilo.karibuni Sana kwaajili ya elimu ya afya ya binadamu.

18/09/2026
18/09/2026

Dr. Luka Mkeni anaeleza namna mapishi ya nyama yanavyoweza kuathiri afya yako.

Kupika nyama kwa joto kali sana, hasa inapofikia zaidi ya 220°C (428°F), kunaweza kuongeza uundwaji wa kemikali zinazoitwa Polycyclic Aromatic Hydrocarbons (PAHs). Baadhi ya PAHs zina uwezo wa kusababisha saratani, na kuathiriwa nazo mara kwa mara kumehusishwa na ongezeko la hatari ya baadhi ya saratani, ikiwemo saratani ya utumbo mpana.

Kwa upande mwingine, utafiti uliochapishwa kupitia PubMed Central (PMC) uliochunguza vyakula vilivyopikwa kwa pressure cooker ulionyesha kuwa upikaji wa kawaida wa nyumbani kwa pressure cooker haukuleta tatizo la uundwaji wa furan, kemikali ambayo imeainishwa kuwa inaweza kusababisha saratani.

Aidha, aina ya nyama yenyewe pia ni muhimu. Nyama nyekundu k**a ng’ombe na nyama zilizosindikwa k**a bacon na sausage zimehusishwa na ongezeko la hatari ya saratani ya utumbo mpana kwasababu ya kampaundi K**a heme iron au nitrates zilizoongezwa bila kujali tu namna zinavyopikwa. (Kwa mujibu wa Cancer Research-UK)

Elimika. Chukua hatua kabla mwili haujachoka.

CREDIT: Wasafi Media

Hivi ndio viambata vilivyopigwa marufuku nchini Tanzania kwasababu za kiusalama wa Afya za Watanzania.Baadhi ya viambata...
17/09/2026

Hivi ndio viambata vilivyopigwa marufuku nchini Tanzania kwasababu za kiusalama wa Afya za Watanzania.

Baadhi ya viambata hivi vinafaa kutumiwa K**a dawa kwa cheti maalumu cha daktari lakini baadhi ya viambata hivi ni hatari kwa Afya kwasababu zinaweza kusababisha madhara makubwa kwenye Afya yako.

Viambata hivi vinaweza kusababisha magonjwa K**a Saratani, Magonjwa ya Figo, Stretch marks, kuchubua ngozi, ngozi kusinyaa au kuwa nyembamba, kuondoa ulinzi wa ngozi n.k

K**a utakutana na Kipodozi chenye kiambata moja wapo Achana nacho Afya yako ni muhimu zaidi kuliko muonekano wa muda mfupi!

ELIMIKA, HAMASIKA, CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA!

17/09/2026

DR. LUKA MKENI anaeleza kuhusu uwepo wa kemikali zinazoweza kuzalishwa wakati wa upikaji na usindikaji wa nyama, ambazo zimehusishwa na ongezeko la hatari ya saratani, ikiwemo saratani ya utumbo mpana.

Upikaji wa nyama kwa joto kali, hasa kuchoma, kuoka au kukaanga, unaweza kuzalisha kemikali k**a Polycyclic Aromatic Hydrocarbons (PAHs) na Heterocyclic Amines (HCAs).

Aidha, nyama zilizosindikwa k**a sausage zinaweza kuwa na misombo ya N-nitroso, ikiwemo nitrosamines, ambayo imehusishwa na hatari ya saratani.

Hivyo, aina ya nyama, kiasi kinacholiwa na namna inavyopikwa au kusindikwa ni mambo muhimu ya kuzingatia katika ulaji wa nyama.

Aidha, Kumbuka kuwa kwa mujibu wa GLOBOCAN 2022, Saratani ya Utumbo mpana ni saratani inayoshika nafasi ya 5 katika orodha ya saratani zinazoongoza nchini Tanzania huku saratani ya Shingo ya kizazi ikiongoza kwa wanawake na saratani ya tezi dume ikiongoza kwa wanaume.

ELIMIKA, HAMASIKA, CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA!

CREDIT: wasafiMedia & Dr Luca Mkeni

Magonjwa ambayo ni silent killers ni 1. Shinikizo la juu la damu (hypertension)2. Kisukari 3. Saratani4. Ugonjwa sugu wa...
17/09/2026

Magonjwa ambayo ni silent killers ni
1. Shinikizo la juu la damu (hypertension)
2. Kisukari
3. Saratani
4. Ugonjwa sugu wa figo (CKD)
5. Shambulio la moyo (heart attack)
6. Rehemu nyingi kwenye damu (hyperlipidemia)

CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA!

16/09/2026

Dr. Samwel Rweyemamu, bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka JKCI, anaeleza kuhusu presha kushuka (Hypotension).

Kwa kawaida, presha ya damu ikiwa chini ya 90/60 mmHg inaweza kuashiria hypotension, hasa ikiwa inaambatana na dalili k**a kizunguzungu, udhaifu au kuzimia.

Sababu zinaweza kuwa upungufu wa maji mwilini, baadhi ya dawa za presha, magonjwa ya moyo, kupoteza damu nyingi au maambukizi makali.

Ukipata presha ya kushuka mara kwa mara, muone mtaalamu wa afya ili kubaini chanzo.

ELIMIKA, HAMASIKA, CHUKUA HATUA KABLA MWILI HAUJACHOKA!

CHANZO: UTV

🇹🇿

Address

Gongo La Mboto
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Health_farm_tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Health_farm_tz:

Shortcuts

Share