Marie Stopes Tanzania

Directions Website Contact the business

Marie Stopes Tanzania Providing Choices in Family Planning and Reproductive Healthcare throughout Tanzania

Marie Stopes Tanzania (MSt), an affiliate partner of MSI, was established in 1987 as a locally registered NGO. It is Tanzania's largest and most specialised sexual reproductive health (SRH) and family planning (FP) organisation and is renowned for providing a wide range of high quality, affordable and client-centred SRH services and information to men, women and young people throughout Tanzania. Through its mobile outreach units alone, MST provides approximately 65% of all long acting and permanent (LAPM) family planning methods in the country. MST is a key implementing partner of the MoH, particularly the Division of Reproductive Health both at central and district levels. MST’s programme is aligned and fully supports the division of reproductive health’s health plans including the National Health Sector Plan, the Community Health Strategy, the Reproductive Health Strategy and the Adolescent Reproductive Health and Development Policy Plan of Action.

Matumizi sahihi ya njia za uzazi wa mpango yatakusaidia kuweka malengo yako ya familia kwa sasa na baadaye. Ndiyo maana ...
10/11/2026

Matumizi sahihi ya njia za uzazi wa mpango yatakusaidia kuweka malengo yako ya familia kwa sasa na baadaye.

Ndiyo maana hakuna njia moja inayomfaa kila mtu, iwe unatafuta njia ya muda mfupi au muda mrefu.

Wataalamu wetu wako tayari kukusaidia kupata njia inayoendana na mahitaji yako. Fanya uchaguzi sahihi leo kisha wasiliana nasi.

📞 𝐏𝐢𝐠𝐚 𝐁𝐮𝐫𝐞: 𝟎𝟖𝟎𝟎 𝟕𝟓𝟑 𝟑𝟑𝟑
📱 𝐖𝐡𝐚𝐭𝐬𝐀𝐩𝐩: 𝟎𝟕𝟓𝟓 𝟖𝟗𝟔 𝟗𝟗𝟔



#𝐌𝐚𝐫𝐢𝐞𝐒𝐭𝐨𝐩𝐞𝐬𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚: #𝐀𝐟𝐲𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨𝐂𝐡𝐚𝐠𝐮𝐨𝐋𝐚𝐤𝐨𝐇𝐚𝐭𝐦𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨.

Ikiwa unajaribu kupata ujauzito bila mafanikio, usikate tamaa wala kuhitimisha haraka kuwa una changamoto ya uzazi. Faha...
09/11/2026

Ikiwa unajaribu kupata ujauzito bila mafanikio, usikate tamaa wala kuhitimisha haraka kuwa una changamoto ya uzazi.

Fahamu mzunguko wako wa hedhi na tambua siku ambazo una uwezekano mkubwa wa kushika ujauzito. Hii inaweza kukusaidia kuelewa vizuri zaidi afya yako ya uzazi.

Kumbuka, umri ni jambo muhimu katika kutafuta ujauzito. Kwa mwanamke mwenye umri chini ya miaka 35, inashauriwa kupata tathmini ya uzazi baada ya mwaka mmoja wa kujaribu kupata ujauzito bila mafanikio. Kwa mwenye umri wa miaka 35 au zaidi, tathmini inashauriwa baada ya miezi sita. Hata hivyo, ikiwa una historia ya matatizo ya uzazi au changamoto nyingine za kiafya, ni vyema kutafuta ushauri wa kitaalamu mapema.

Changamoto za kupata ujauzito zinaweza kumpata mwanamke au mwanaume. Hivyo, ni muhimu wote wawili kushiriki katika uchunguzi ili kubaini chanzo na kupata ushauri sahihi.

📞 𝐏𝐢𝐠𝐚 𝐁𝐮𝐫𝐞: 𝟎𝟖𝟎𝟎 𝟕𝟓𝟑 𝟑𝟑𝟑
📱 𝐖𝐡𝐚𝐭𝐬𝐀𝐩𝐩: 𝟎𝟕𝟓𝟓 𝟖𝟗𝟔 𝟗𝟗𝟔



#𝐌𝐚𝐫𝐢𝐞𝐒𝐭𝐨𝐩𝐞𝐬𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚: - #𝐀𝐟𝐲𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨𝐂𝐡𝐚𝐠𝐮𝐨𝐋𝐚𝐤𝐨𝐇𝐚𝐭𝐦𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨.

04/11/2026

Unapata ovulation kila mwezi lakini bado hujapata ujauzito?

Kuwa na ovulation pekee siyo dhamana ya kupata ujauzito. Wakati mwingine changamoto zinaweza kuwa kwa mwanamke, mwanaume au wote wawili.

Usibaki na maswali au kukata tamaa. Uchunguzi wa mapema unaweza kusaidia kubaini chanzo na kukupa mwongozo sahihi wa kitaalamu.

Karibu Marie Stopes Mwenge kwa ushauri na huduma za afya ya uzazi.

📞 𝐏𝐢𝐠𝐚 𝐁𝐮𝐫𝐞: 𝟎𝟖𝟎𝟎 𝟕𝟓𝟑 𝟑𝟑𝟑
📱 𝐖𝐡𝐚𝐭𝐬𝐀𝐩𝐩: 𝟎𝟕𝟓𝟓 𝟖𝟗𝟔 𝟗𝟗𝟔



#𝐌𝐚𝐫𝐢𝐞𝐒𝐭𝐨𝐩𝐞𝐬𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚: - #𝐀𝐟𝐲𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨𝐂𝐡𝐚𝐠𝐮𝐨𝐋𝐚𝐤𝐨𝐇𝐚𝐭𝐦𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨.

Karibu Novemba, Mwezi wa Afya ya Uzazi.Mwezi huu, tuungane kujifunza, kuuliza maswali na kupata taarifa sahihi kutoka kw...
02/11/2026

Karibu Novemba, Mwezi wa Afya ya Uzazi.

Mwezi huu, tuungane kujifunza, kuuliza maswali na kupata taarifa sahihi kutoka kwa wataalamu wa afya.

𝐔𝐧𝐚 𝐬𝐰𝐚𝐥𝐢 𝐤𝐮𝐡𝐮𝐬𝐮 𝐚𝐟𝐲𝐚 𝐲𝐚 𝐮𝐳𝐚𝐳𝐢? 𝐓𝐞𝐦𝐛𝐞𝐥𝐞𝐚 𝐤𝐢𝐭𝐮𝐨 𝐜𝐡𝐞𝐭𝐮 𝐤𝐢𝐥𝐢𝐜𝐡𝐨 𝐤𝐚𝐫𝐢𝐛𝐮 𝐧𝐚𝐰𝐞 𝐚𝐮 𝐰𝐚𝐬𝐢𝐥𝐢𝐚𝐧𝐚 𝐧𝐚𝐬𝐢 𝐤𝐰𝐚;

📞 𝐏𝐢𝐠𝐚 𝐁𝐮𝐫𝐞: 𝟎𝟖𝟎𝟎 𝟕𝟓𝟑 𝟑𝟑𝟑
📱 𝐖𝐡𝐚𝐭𝐬𝐀𝐩𝐩: 𝟎𝟕𝟓𝟓 𝟖𝟗𝟔 𝟗𝟗𝟔



#𝐌𝐚𝐫𝐢𝐞𝐒𝐭𝐨𝐩𝐞𝐬𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚: - #𝐀𝐟𝐲𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨𝐂𝐡𝐚𝐠𝐮𝐨𝐋𝐚𝐤𝐨𝐇𝐚𝐭𝐦𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨.

29/10/2026

Unapanga kushika Ujauzito na hujui uanzie wapi?

Katika hospitali yetu, tuna famasi yenye dawa na virutubisho mbalimbali kwa mahitaji tofauti ya afya, ikiwemo virutubisho vinavyoweza kupendekezwa wakati wa kujiandaa kupata ujauzito.

Pia, una nafasi ya kuonana na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, ambaye atakushauri kulingana na mahitaji yako, kukusaidia kujiandaa kwa ujauzito na kutathmini changamoto zinazoweza kuathiri uwezo wa kushika mimba pale inapohitajika.

Usitumie dawa au virutubisho kwa mazoea bila ushauri wa kitaalamu.

Tembelea hospitali yetu leo kwa ushauri na tathmini ya afya yako ya uzazi.
📞 𝐏𝐢𝐠𝐚 𝐁𝐮𝐫𝐞: 𝟎𝟖𝟎𝟎 𝟕𝟓𝟑 𝟑𝟑𝟑
📱 𝐖𝐡𝐚𝐭𝐬𝐀𝐩𝐩: 𝟎𝟕𝟓𝟓 𝟖𝟗𝟔 𝟗𝟗𝟔



#𝐌𝐚𝐫𝐢𝐞𝐒𝐭𝐨𝐩𝐞𝐬𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚: - #𝐀𝐟𝐲𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨𝐂𝐡𝐚𝐠𝐮𝐨𝐋𝐚𝐤𝐨𝐇𝐚𝐭𝐦𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨.

Kila kijana anastahili kupata taarifa sahihi za afya ya uzazi.Taarifa sahihi zinakupa uwezo wa kufanya maamuzi sahihi, k...
27/10/2026

Kila kijana anastahili kupata taarifa sahihi za afya ya uzazi.

Taarifa sahihi zinakupa uwezo wa kufanya maamuzi sahihi, kulinda afya yako na kufikia malengo yako ya maisha.

Tembelea kituo chetu kilicho karibu nawe kwa ushauri na huduma rafiki kwa vijana.
𝐏𝐢𝐠𝐚 𝐁𝐮𝐫𝐞: 𝟎𝟖𝟎𝟎 𝟕𝟓𝟑 𝟑𝟑𝟑
𝐖𝐡𝐚𝐭𝐬𝐀𝐩𝐩: 𝟎𝟕𝟓𝟓 𝟖𝟗𝟔 𝟗𝟗𝟔



#𝐌𝐚𝐫𝐢𝐞𝐒𝐭𝐨𝐩𝐞𝐬𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚: - #𝐀𝐟𝐲𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨𝐂𝐡𝐚𝐠𝐮𝐨𝐋𝐚𝐤𝐨𝐇𝐚𝐭𝐦𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨.

26/10/2026

Folic Acid ni virutubisho ambavyo vina mchango mkubwa katika ukuaji wa ubongo na uundaji wa uti wa mgongo wa mtoto akiwa tumboni.

Kwa mama anayetarajia kupata ujauzito au tayari ni mjamzito, kupata taarifa sahihi kuhusu Folic Acid ni hatua muhimu katika kulinda afya ya mtoto.

Tazama video hii daktari akieleza umuhimu wa Folic Acid.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa

𝐏𝐢𝐠𝐚 𝐁𝐮𝐫𝐞: 𝟎𝟖𝟎𝟎 𝟕𝟓𝟑 𝟑𝟑𝟑
𝐖𝐡𝐚𝐭𝐬𝐀𝐩𝐩: 𝟎𝟕𝟓𝟓 𝟖𝟗𝟔 𝟗𝟗𝟔



#𝐌𝐚𝐫𝐢𝐞𝐒𝐭𝐨𝐩𝐞𝐬𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚: - #𝐀𝐟𝐲𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨𝐂𝐡𝐚𝐠𝐮𝐨𝐋𝐚𝐤𝐨𝐇𝐚𝐭𝐦𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨.

Marie Stopes Tanzania tunajivunia kufanya kazi na kampuni mbalimbali za bima ya afya lengo ni kuhakikisha huduma za afya...
23/10/2026

Marie Stopes Tanzania tunajivunia kufanya kazi na kampuni mbalimbali za bima ya afya lengo ni kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wote.

Hizi ni baadhi ya kampuni za bima za afya zinazopokelewa kwenye vituo vyetu vya Afya vinavopatikana Dar es salaam, Arusha, Mwanza, Musoma, Iringa, Makambako na Zanzibar.

𝐓𝐮𝐭𝐞𝐦𝐛𝐞𝐥𝐞𝐞 𝐥𝐞𝐨 𝐤𝐮𝐩𝐚𝐭𝐚 𝐡𝐮𝐝𝐮𝐦𝐚 𝐚𝐮 𝐰𝐚𝐬𝐢𝐥𝐢𝐚𝐧𝐚 𝐧𝐚𝐬𝐢 𝐤𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐰𝐞𝐤𝐚 𝐦𝐢𝐚𝐝𝐢 𝐲𝐚𝐤𝐨.

𝐏𝐢𝐠𝐚 𝐁𝐮𝐫𝐞: 𝟎𝟖𝟎𝟎 𝟕𝟓𝟑 𝟑𝟑𝟑
𝐖𝐡𝐚𝐭𝐬𝐀𝐩𝐩: 𝟎𝟕𝟓𝟓 𝟖𝟗𝟔 𝟗𝟗𝟔

#𝐀𝐟𝐲𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨𝐂𝐡𝐚𝐠𝐮𝐨𝐋𝐚𝐤𝐨𝐇𝐚𝐭𝐦𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨

#𝐌𝐚𝐫𝐢𝐞𝐒𝐭𝐨𝐩𝐞𝐬𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚: - #𝐀𝐟𝐲𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨𝐂𝐡𝐚𝐠𝐮𝐨𝐋𝐚𝐤𝐨𝐇𝐚𝐭𝐦𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨.

22/10/2026

Maboresho yanaendelea katika Hospitali yetu ya Marie Stopes Mwenge, na mradi umefikia hatua nzuri kuelekea kukamilika.

Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa, pamoja na shughuli za ukarabati zinazoendelea, huduma za afya zinaendelea kutolewa k**a kawaida kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 1:00 jioni.

Huduma muhimu za afya bado zinapatikana kwa ubora, usalama na faragha ile ile mnayoifahamu kutoka kwetu.

Lengo la maboresho haya ni kuhakikisha kuwa katika siku zijazo mnapata huduma katika mazingira bora zaidi, ya kisasa na yanayozingatia mahitaji ya kila mtu.

𝐊𝐮𝐰𝐞𝐤𝐚 𝐦𝐢𝐚𝐝𝐢 𝐚𝐮 𝐤𝐮𝐩𝐚𝐭𝐚 𝐭𝐚𝐚𝐫𝐢𝐟𝐚 𝐳𝐚𝐢𝐝𝐢 𝐤𝐮𝐡𝐮𝐬𝐮 𝐮𝐤𝐚𝐫𝐚𝐛𝐚𝐭𝐢 𝐡𝐮𝐮 𝐰𝐚𝐬𝐢𝐥𝐢𝐚𝐧𝐚 𝐧𝐚𝐬𝐢,

𝐏𝐢𝐠𝐚 𝐁𝐮𝐫𝐞 𝟎𝟖𝟎𝟎 𝟕𝟓𝟑 𝟑𝟑𝟑:
𝐖𝐡𝐚𝐭𝐬𝐀𝐩𝐩: 𝟎𝟕𝟓𝟓 𝟖𝟗𝟔 𝟗𝟗𝟔



#𝐌𝐚𝐫𝐢𝐞𝐒𝐭𝐨𝐩𝐞𝐬𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚: - #𝐀𝐟𝐲𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨𝐂𝐡𝐚𝐠𝐮𝐨𝐋𝐚𝐤𝐨𝐇𝐚𝐭𝐦𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨.

Kulinda afya ya matiti yako huanza na hatua unazochukua leo.Fahamu mabadiliko yanayotokea kwenye matiti yako na usisite ...
21/10/2026

Kulinda afya ya matiti yako huanza na hatua unazochukua leo.

Fahamu mabadiliko yanayotokea kwenye matiti yako na usisite kutafuta ushauri wa kitaalamu ikiwa kuna jambo jipya au linalokutia wasiwasi.

Uchunguzi wa mapema unaweza kuleta tofauti kubwa.

Kwa taarifa au ushauri zaidi, wasiliana nasi kupitia:
𝐏𝐢𝐠𝐚 𝐁𝐮𝐫𝐞 𝟎𝟖𝟎𝟎 𝟕𝟓𝟑 𝟑𝟑𝟑:
𝐖𝐡𝐚𝐭𝐬𝐀𝐩𝐩: 𝟎𝟕𝟓𝟓 𝟖𝟗𝟔 𝟗𝟗𝟔



#𝐌𝐚𝐫𝐢𝐞𝐒𝐭𝐨𝐩𝐞𝐬𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚: - #𝐀𝐟𝐲𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨𝐂𝐡𝐚𝐠𝐮𝐨𝐋𝐚𝐤𝐨𝐇𝐚𝐭𝐦𝐚𝐘𝐚𝐤𝐨.

Address

Mwenge
Dar Es Salaam
11000

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Marie Stopes Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Marie Stopes Tanzania:

Shortcuts

Share

Nearby health & beauty businesses